UBORESHAJI MIUNDOMBINU YA MAJISAFI
18 Apr, 2024
Kazi ya uboreshaji wa miundombinu ya majisafi ili kudhibiti upotevu wa maji katika bomba yenye ukubwa wa inchi 2 inaendelea katika eneo la Kaole Kata Bagamoyo Mjini chini ya usimamizi wa mafundi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA).
Utekelezaji wa kazi hii unalenga kuimarisha huduma katika maeneo ya Kaole, Kidogo chekundu,Nianjema, Kilomo pamoja na Mtambani kwa kuwapatia huduma bora na yakutosheleza wakati wote.