UBORESHAJI MIUNDOMBINU TEGETA KWA NDEVU - KINONDONI
19 Mar, 2024
Kazi ya uboreshaji wa miundombinu ya majisafi ili kudhibiti upotevu wa maji katika bomba yenye ukubwa wa inchi 4 ikifanyika katika eneo la Tegeta kwa ndevu darajani chini ya usimamizi wa mafundi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA).
Utekelezaji wa kazi hii unalenga kuimarisha huduma katika maeneo ya JKT, Siksa, Kiaroni, Meco, Jeshini, Kilumbi, Rc meco, pamoja na Uyoga kichuguu cha jeshi kwa kuwapatia huduma bora na yakutosheleza wakati wote.