Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
UBORESHAJI DIRA ZA MAJI KUSAIDIA KULETA UFANISI WA HUDUMA - KINONDONI
10 Feb, 2024
UBORESHAJI DIRA ZA MAJI KUSAIDIA KULETA UFANISI WA HUDUMA - KINONDONI

Mafundi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) mkoa wa kihuduma Kinondoni wakiendelea na zoezi la kukagua dira za maji pamoja na kunyanyua juu mita katika makazi ya wateja ambazo ziko ndani ya eneo la kihuduma.

Zoezi hilo linaendelea kutekelezwa ambapo mita 140 zimekaguliwa katika maeneo ya Masaki, Mkwajuni, Msasani, Coco beach, Victoria, Mikocheni, Block 41 na Mwananyamala.

Lengo la ukaguzi wa dira za maji wa mara kwa mara ni kuhakikisha ufanisi mzuri wa mita hizo, kudhibiti upotevu wa maji pamoja na kurahisisha usomaji wa mita kwa mteja na watumishi wa DAWASA.