TEGETA 'A' HADI MADALE WAITWA MAUNGANISHO HUDUMA YA MAJI - KINONDONI
16 Feb, 2024
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) inawataarifu wakazi wa maeneo ya Goba, Tegeta A, Kulangwa, Muungano, Kilimahewa, Kilimahewa juu, Kisanga, Wazo, Nyakasangwe, Salasala kwa Babu, Madale, Goba Mpakani, Majengo na Kinzudi kuwa inaendelea na zoezi la ugawaji na utoaji wa vifaa vya maunganisho mapya ya huduma ya majisafi kupitia ofisi ya kihuduma DAWASA Mivumoni
Sambamba na zoezi hilo, elimu ya huduma za maji, njia za malipo pamoja na mawasiliano na Mamlaka zinatolewa kwa wateja wapya.
Takribani Wananchi 200 katika maeneo tajwa watanufaika na huduma ya majisafi baada ya maunganisho kukamilika.
Endelea kuwasiliana na DAWASA kupitia kituo cha huduma kwa wateja namba 0800110064 (Bure) au 0734 355 755 (DAWASA Mivumoni).