TEGETA A, GOBA, MADALE KAZI INAENDELEA
15 Sep, 2023
Kazi ya uchimbaji na ulazaji wa bomba za inchi 3, 2, na 1 ikiendelea katika maeneo ya Tegeta A, Goba na Madale kwa umbali wa kilomita 3.5 ili kusogeza huduma kwa wateja waliopo nje ya mita 50 kutoka kwenye bomba kuu.
Kukamilika kwa kazi hii kutanufaisha zaidi ya wateja 400 katika maeneo hayo kwa kupata huduma bora ya Majisafi.