Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
SERIKALI KUBORESHA  HUDUMA YA MAJI MANGA - HANDENI
23 Feb, 2024
SERIKALI KUBORESHA  HUDUMA YA MAJI MANGA - HANDENI

Timu ya wataalamu kutoka Wizara ya Maji imetembelea Kijiji cha Manga wilayani Handeni kwa lengo la kukagua na kuandaa mpango mkakati  wa uboreshaji huduma ya majisafi kwa wakazi takribani 100,000.

Wataalamu hao kwa kushirikiana na DAWASA wamejadili hatua za muda mrefu na muda mfupi za kuwapatia wananchi huduma ya maji ili waondokane na adha upatikanaji wa huduma ya maji kwa msukumo mdogo inayosababishwa na changamoto za  kijiographia huku mipango ya muda mrefu ikiendelea kusukwa.

Mkurugenzi Msaidizi idara ya uzalishaji na usambazaji Maji, Wizara ya Maji Mhandisi Leornard Msenyele ameipongeza DAWASA kwa usimamizi  wa huduma katika eneo kupitia Mradi wa Chalinze awamu ya tatu na kusisitiza Mamlaka kufanyia kazi mpango walioujadili kwa pamoja ili wananchi waanze kupata maji  mara moja.

" Kwanza kabisa tunawapongeza DAWASA kwa kazi nzuri na pia tumefarijika kuona tayari Mamlaka ilianza kuandaa mikakati ya kuondokana na changamoto hii,  tunawasihi kuanza kufanyia kazi yale ambayo tumeyajadili ili wananchi wapate huduma" amesema Mhandisi Msenyele.

Kwa upande wake Meneja wa Mkoa wa Kihuduma DAWASA Chalinze, Mhandisi Felchesm Kimaro amesema ujio wa wataalamu kutoka Wizarani utasaidia kuboresha mipango iliyokuwepo ya kuboresha huduma ikiwa ni pamoja na kufunga pampu ndogo ya ndani kusukuma maji yaani (submissible pump)

" Tunawashukuru  kwa kufika kijiji cha Manga,  tumepata mawazo mazuri mpya sasa ni wakati wa utekelezaji tumepokea na kuendelea kutimiza jukumu letu la kuhudumia wananchi"  amesema Mhandisi Kimaro.

Naye, Mwenyekiti wa Kijiji cha Manga kwa niaba ya wananchi Ndugu Luizo Omari amewashukuru wataalam kwa ujio huo kwani unatoa matumaini ya kuisha kwa adha ya upatikanaji wa maji na kupunguza malalamiko kutoka kwa wananchi kuwa gharama za maji ni ghali na maji ya visima yanayopatikana sio salama kwa afya.

Kijiji cha Manga kinahudumiwa na DAWASA kupitia Mkoa wa Kihuduma Chalinze ni moja ya wanufaika wa Mradi wa Chalinze awamu ya tatu.