SARANGA NA KIFURU WAITWA MAUNGANISHO YA MAJI
15 Sep, 2023
Habari njema kwa wakazi walioomba huduma ya maji katika maeneo ya Saranga na Kifuru katika kata ya Saranga kuwa ofisi za DAWASA KINYEREZI inaendelea na zoezi la utoaji wa vifaa vya maunganisho mapya ya huduma ya majisafi.
Pamoja na zoezi hilo, elimu mbalimbali zinatolewa ikiwa ni pamoja na elimu ya utunzaji miundombinu ya maji, matumizi sahihi ya maji, njia rasmi za mawasiliano na malipo ya ankara na huduma nyingine zitolewazo na DAWASA.
Zaidi ya wateja 200 wa maeneo hayo wanatarajia kuanza kunufaika na huduma ya majisafi.
Kwa msaada na taarifa zaidi wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja namba 0800110064 (Bure) au 0734 455 755 (DAWASA Kinyerezi)