POLISI WAFUGIWA DIRA ZA MAJI ZA MALIPO YA KABLA
18 Apr, 2024
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) imefunga mita takribani 50 za huduma ya malipo ya kabla (Pre-paid meters) katika makazi ya watumishi wa Jeshi la Polisi Oysterbay Wilaya ya Kinondoni ikiwa ni muendelezo wa matumizi ya mita za kabla kwa wateja wa Mkoa wa Dar es salaam.
Ufungaji wa mita ni wa majaribio kwa lengo la kuangalia na kupima ufanisi wake kuelekea mabadiliko ya kuanza kutumia rasmi mita za huduma ya malipo ya kabla.