NI MWENDO WA MAUNGANISHO YA HUDUMA YA MAJI KWA WAKAZI UBUNGO
06 Sep, 2023
Habari njema kwa wakazi wote wa Kata za Mbezi, Kwembe, Msigani, Kibamba na Kiluvya Wilaya ya Ubungo kuwa ofisi za *DAWASA KIBAMBA * inaendelea na zoezi la utoaji wa vifaa vya maunganisho mapya ya huduma ya majisafi.
Utoaji wa vifaa vya maunganisho mapya huendana sambamba na utoaji wa elimu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na elimu ya utunzaji miundombinu ya maji, matumizi sahihi ya maji, njia rasmi za mawasiliano, njia za malipo ya ankara na huduma nyingine zitolewazo na DAWASA.
Kwa msaada na taarifa zaidi wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja 0800110064 (Bure) na 0734 460 022 (DAWASA Kibamba)