Naibu Waziri wa Maji, Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi amewasili kwenye Ofisi za DAWASA
04 Sep, 2023
Naibu Waziri wa Maji, Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi amewasili kwenye Ofisi za DAWASA na kupokea taarifa ya hali ya Upatikanaji wa huduma ya maji katika Mkoa wa Dar es Salaam kutoka kwa Kaimu Mtendaji wa DAWASA Mhandisi Shabani Mkwanywe. Mhe Maryprisca yupo katika ziara ya Siku tatu kutembelea na kukagua utekelezaji wa miradi ya majisafi na usafi wa mazingira Mkoa wa Dar es salaam.
Mhe. Maryprisca amepokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Saad Mtambuli.