Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
NAIBU SPIKA ASISITIZA UTUNZAJI WA MIUNDOMBINU YA MAJISAFI
15 Sep, 2023
NAIBU SPIKA ASISITIZA UTUNZAJI WA MIUNDOMBINU YA MAJISAFI

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungani wa Tanzania na Mbunge wa Jimbo la Ilala Mhe. Mussa Azzan Zungu amewataka wakazi wa maeneo ya Mchikichini na Mheza B wa Kata ya Mchikichini kutunza miundombinu ya Maji na kuongeza vifaa vya kuhifadhi maji pindi huduma inapopungua.

Ameyasema hayo alipotembelea maeneo yenye changamoto ya upatikanaji wa maji katika jimbo lake akiambatana na watumishi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) na kushuhudia zoezi la kuboresha miundombinu kwa kubadilisha bomba la inchi 3/4 na kuweka bomba la inchi 1.5 kwa umbali wa mita 300, ili kuboresha hali ya upatikanaji wa maji kwa wakazi zaidi ya 140.