Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
NAIBU KATIBU MKUU ATEMBELEA MIRADI YA DAWASA
13 Feb, 2024
NAIBU KATIBU MKUU ATEMBELEA MIRADI YA DAWASA

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji , Mhandisi Mwajuma Waziri yuko katika ziara ya siku moja kutembelea na kukagua miradi mbalimbali inayosimamiwa na kutekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA).


Miongoni mwa miradi hiyo ni pamoja na Mradi wa uendelezaji visima eneo la Kigamboni, Mradi wa Usafi wa Mazingira eneo la Mbezi Beach na mitambo ya uzalishaji Maji Ruvu Chini na Ruvu Juu iliyopo Bagamoyo na Mlandizi Mkoani Pwani.