MWANALUGALI WABORESHEWA HUDUMA ZA MAJI - KIBAHA
19 Mar, 2024
Kazi ya kutoa toleo la inchi 4 katika bomba la inchi 48 ikitekelezwa na mafundi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Kibaha katika eneo la Shirika la Elimu kwa lengo la kuboresha huduma ya maji kwa wakazi wa kata ya Tumbi, mtaa wa Mwanalugali, Mkoa wa Pwani.
Kukamilika kwa kazi hii kutaongeza upatikanaji wa huduma bora kwa wakazi wa mtaa wa Mwanalugali, Oysterbay na Msikitini.