MRADI WA USAFI WA MAZINGIRA PSSSF KAZI INAENDELEA
06 Sep, 2023
Kazi ya uchimbaji na ulazaji wa bomba za mtandao wa majitaka zenye ukubwa wa inchi 10 ikiendelea eneo la Sinza Mori Jijini Dar es salaam ikiwa sehemu ya utekelezaji wa mradi wa Usafi wa Mazingira PSSSF Sinza-Kijitonyama.
Mradi wa Usafi wa Mazingira PSSSF Sinza-Kijitonyama umefikia asilimia 30 ya utekelezaji wake na unategemea kukamilika ifikapo mwishoni mwa mwezi Septemba 2023 huku ukienda kunufaisha zaidi ya wateja 1000.