"MRADI WA UJENZI WA VITUO VYA KUTOA HUDUMA KWA UMMA UIGWE NA WENGINE." - PROF KATUNDU
Katibu Mkuu Wizara ya maji Profesa Jamal Katundu amefurahishwa na mradi wa ujenzi wa vituo vya kutoa huduma uliotekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) wenye lengo la kuboresha mazingira na kuzihasa Mamlaka za maji nchini kuiga mfano huo kwa DAWASA.
Profesa Katundu ameyasema hayo alipotembelea banda la elimu kwa umma la DAWASA katika Kongamano la kimataifa la kisayansi la maji lililoambatana na maadhimisho ya miaka 50 ya Chuo cha Maji.
"Nimeona mradi huu mzuri na bora kabisa, mradi uliolenga kuboresha usafi wa mazingira huu ni mfano wa kuigwa, na nitoe rai sasa kwa Mamlaka za maji nchini kuiga mfano huu toka DAWASA kwa kuja kujifunza na kutekeleza katika maeneo yao" ameeleza Profesa Katundu.
Akielezea utekelezaji wa mradi huo, Kaimu mkuu wa kitengo cha Mawasiliano DAWASA , Everlasting Lyaro amesema Mamlaka imejenga vituo vya umma 30 katika wilaya zote tano katika Mkoa wa Dar es salaam na katika maeneo yenye mkusanyiko wa watu kama vile Sokon, katika standi za magari ili kuwafikia wananchi wengi zaidi.