MNARANI KISARAWE WABORESHEWA HUDUMA
22 Apr, 2024
Utekelezaji wa kazi ya maboresho ya miundombinu ya usambazaji maji katika eneo la Mnarani, Wilaya ya Kisarawe imekamilishwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kwa lengo la kuimarisha upatikanaji wa huduma kwa wakazi wa Kata za Kisarawe na Pugu.
Kazi hiyo imehusisha unasuaji wa valvu ya inchi 16 iliyojifunga na kusababisha kutopitisha maji hivyo kupelekea baadhi ya wakazi kukosa huduma ya maji.
Kukamilika kwa kazi hiyo kutaimarisha upatikanaji wa huduma ya maji kwa wakazi zaidi ya 3,000 waliopo katika mitaa ya Matumbini, Bomani, Kimani, Kibaoni A&B, Sanze, Vigama, Vigungu, Ng'ere na baadhi ya maeneo ya Mgeure Juu ikiwemo Kwakoka na Buyuni.