MKURANGA YAWAITA WANANCHI WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA
09 Oct, 2023
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kupitia Mkoa wa kihuduma DAWASA Mkuranga katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja imesogeza huduma karibu zaidi na wananchi kwa kufungua madawati ya huduma kwa wateja katika ofisi za Serikali ya Kijiji cha Mkuranga ili kusikiliza changamoto pamoja na kupokea maombi ya maunganisho mapya ya maji kutoka kwa wateja.
Ofisi ya DAWASA Mkuranga itaendelea na zoezi la kuwasikiliza wateja kwa mwezi mzima kwa kufungua madawati ya huduma kwa wateja katika ofisi za Serikali ya Kijiji cha Vianzi, Mwandege na Mwanambaya.