Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
MKOMBOZI, MWEMBE-MKOLE HADI MANZESE MVULENI WABORESHEWA HUDUMA YA MAJI
24 Apr, 2024
MKOMBOZI, MWEMBE-MKOLE HADI MANZESE MVULENI WABORESHEWA HUDUMA YA MAJI

Kazi ya maboresho ya miundombinu ya majisafi kwa kutekeleza kazi ya kulaza bomba la inchi 4 kwa umbali wa mita 150 ikiendelea kupitia mkoa wa kihuduma DAWASA - Magomeni.

Utekelezaji wa kazi hii utaboresha huduma kwa kuongeza msukumo wa maji kwa wakazi wapatao 280 wa maeneo ya Mkombozi, mwembemkole, tupendane na baadhi ya maeneo ya Manzese - mvuleni.

DAWASA inaendelea kuwasihi wananchi kutoa taarifa za mara kwa mara endapo watabaini uvujaji katika maeneo yao kupitia kituo cha huduma kwa wateja namba 0800110064 (Bure) na mitandao ya kijamii ya mamlaka.