MIUNDOMBINU ILIYOATHIRIKA NA MVUA YAKARABATIWA MBEZI
02 Feb, 2024
Kazi ya kudhibiti upotevu wa maji katika bomba la usambazaji maji lenye ukubwa wa inchi 30 katika eneo Mbezi Luis inaendelea kutekelezwa na mafundi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA)
Kazi hiyo inafanyika kutokana na athari za mvua na inahusisha kuziba kipande cha bomba kilichoathirika.
Kukamilika kwa kazi hiyo kutarejesha huduma kwa wakazi wa maeneo ya Stendi ya Magufuli, Kiyopeni, Luguruni, Makabe, Mbezi Luis na Kibamba.