MAWENI KAZI INAENDELEA - KIGAMBONI
19 Mar, 2024
Kazi ya matengenezo ya bomba kuu la usambazaji maji lenye ukubwa wa inchi 16 ikiendelea kutekelezwa na mafundi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) eneo la Maweni, Wilayani Kigamboni.
Kukamilika kwa matengenezo hayo, kutaboresha upatikanaji wa huduma ya maji kwa wakazi wa maeneo ya Maweni, Kwa Mwingila, Big Stone, Mtaa wa Malaika, Mtaa wa Njukuru, Beach Zone, Aboud Jumbe, Endless na maeneo jirani ya njia panda ya Kijiji Beach.