MATENGENEZO KITUO CHA KUSUKUMA MAJI SEGEREA
15 Sep, 2023
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) kwa kushirikiana na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wanaendelea na zoezi la kufunga transfoma na mita ya umeme katika kituo cha kusukuma maji cha Segerea.
Zoezi hilo limelenga kuongeza ufanisi katika kituo hicho ili kuboresha upatikanaji wa maji kwa wakazi wa maeneo ya Viwanja vya benki, Kokomtama, Sabisa, Kwa Sanga, Magoza na viunga vyake Kata ya Kisukuru.