MABORESHO YA MIUNDOMBINU YA MAJITAKA ILALA
24 Apr, 2024
Kazi ya kubadilisha na kurekebisha bomba chakavu la majitaka lenye ukubwa wa inchi 10 ikiendelea katika eneo la Barabara ya Jamhuri katika kata ya Kivukoni kwa lengo la kuimarisha huduma ya Usafi wa Mazingira katika Wilaya ya Ilala.
Kazi hii inafanyika usiku na mchana na DAWASA ili kuhakikisha huduma ya usafi wa mazingira unaimarika ili kuepukana na uchafuzi wa Mazingira unaoweza kuhatarisha afya za wakazi.