MABORESHO YA MIUNDOMBINU YA MAJI SUKITA
22 Apr, 2024
Kazi ya kudhibiti upotevu wa maji katika bomba la usambazaji maji lenye ukubwa wa inchi 18 katika eneo la Buguruni Sukita wilaya ya Ilala inaendelea kutekelezwa na mafundi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA)
Kazi hiyo imehusisha kuunganisha bomba lilioathiriwa na mvua katika mto Msimbazi
Kukamilika kwa kazi hiyo kutarejesha huduma ya Majisafi kwa wakazi wa maeneo ya Kigogo, Mburahati, Manzese, Buguruni Ghana na Ubungo.