MABORESHO YA HUDUMA YA MAJI MABIBO JESHINI
02 Feb, 2024
Kazi ya matengenezo ya bomba la usambazaji maji la inchi 6 inaendelea kutekelezwa na mafundi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kwa lengo la kudhibiti upotevu wa maji katika eneo la Mabibo jeshini, kata ya Mabibo Wilaya ya Ubungo.
Kukamilika kwa kazi hii kutarudisha huduma ya maji kwa wakazi 300 wa maeneo ya Mabibo farasi, mtaa wa jeshini, mtaa wa kanuni, mtaa wa jitegemee, mtaa wa azimio na Mtaa wa matokeo.