MABORESHO YA HUDUMA YA MAJI KWEMBE NA MBEZI
28 Feb, 2024
Kazi ya kuongeza msukumo wa maji kwenye bomba la usambazaji maji la inchi 16 linalopeleka maji kwenye tenki la Mshikamano inayohusisha ufungaji wa pampu eneo la Mbezi inn na ulazaji wa bomba la inchi 6 kwa umbali wa mita 20 inaendelea kutekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam ( DAWASA).
Kukamilika kwa kazi hiyo kutaboresha huduma kwa wakazi wa Luguruni, Magari saba, Msakuzi, Machimbo, Masaki ndogo, Goodhope, Msakuzi kwa Massawe, Kwa Gamba, Madafu na Miti mirefu.