MABORESHO YA HUDUMA MBEZI MTONI KINONDONI
19 Jan, 2024
MABORESHO YA HUDUMA MBEZI MTONI
Matengenezo ya bomba la inchi 6 ikiendelea kufanyika na mafundi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kupitia mkoa wa kihuduma Kawe kwa lengo la kuboresha hali ya upatikanaji wa huduma ya maji eneo la Mbezi Mtoni, kata ya Mbezi juu Wilaya ya Kinondoni.
Kukamilika kwa kazi hii kutanufaisha wateja 3200 wa maeneo ya Sanya, Mbuyuni, Kwa Nyalala, Shukuru Dispensary, Gold star CCM, Msikitini, Ukololo, Sanya maji chumvi, Frame sita, FPCT Church, Kagoma, Mafuta ya taa na Kwa mama Bob.