Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
MABORESHO YA HUDUMA KIJICHI - MBAGALA
02 Feb, 2024
MABORESHO YA HUDUMA KIJICHI - MBAGALA

Kazi ya upanuzi wa mtandao wa huduma ya majisafi kutoka inchi 1 kwenda inchi mbili na nusu (2.5) kwa lengo la kuongeza msukumo wa maji kwa wakazi wa kata ya Kijichi-Mbagala ikiendelea kutekelezwa na mafundi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA).

Upanuzi huo wa mtandao utaboresha na kuongeza msukumo wa maji kwa wakazi wa maeneo ya Kijichi Pene, Heineken, Mtaa wa Tausi na ofisi ya kata ya Kijichi yaliyokuwa yakipata huduma kwa msukumo mdogo (low pressure).