MABORESHO MIUNDOMBINU YA MAJITAKA - KIJITONYAMA
02 Feb, 2024
Kazi ya maboresho ya bomba la majitaka inchi 24 lililopata hitilafu kutokana na kutitia kwa bomba na kujaa mchanga ikiwa ukingoni mwa utekelezaji wake na mafundi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) katika eneo la Sayansi wilayani Kinondoni Jijini Dar es salaam.
Kumalizia kwa kazi hii kutaboresha huduma ya usafi wa mazingira kwa wananchi wa eneo la Sayansi, Sinza, Mwenge, Kijitonyama, na Mlimani city na maeneo ya jirani na kumaliza changamoto ya utiririkaji majitaka mara kwa mara katika maeneo hayo.