Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
MABORESHO MIUNDOMBINU YA MAJI MPIJI MAGOHE - KINONDONI
18 Mar, 2024
MABORESHO MIUNDOMBINU YA MAJI MPIJI MAGOHE - KINONDONI

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inaendelea na maboresho ya miundombinu ya maji katika eneo la Mpiji katika kata ya Mbweni Wilaya ya Kinondoni.

Kupitia Mkandarasi DB SHAPRIYA & CO LIMITED inatekeleza maboresho hayo yanayohusisha kazi ya kuunga bomba kubwa la kusambaza maji la inchi 54 lililoathiriwa na mvua.

Akizungumzia utekelezaji wa zoezi hilo, Mhandisi Haika Temba amesema kuwa kazi inayoendelea sasa ni kutoa bomba la inchi 54 kutoka mtoni na kulichomelea.

"Kazi hii ni endelevu ambapo mpaka sasa kazi ya kuchimba na kutoa maji kwa lengo la kutoa bomba mtoni inaendelea. Lengo ni kuhakikisha huduma ya maji inaimarika katika maeneo ya Kerege, Mapinga, Mbweni, Tegeta, Bunju Beach, Boko hadi Ununio" amesema.

Mhandisi Haika ameongeza kuwa kazi hiyo inatekelezwa kwa kasi ili kukamilisha haraka matengenezo hayo kabla ya kuanza kwa msimu wa mvua kubwa uliotangazwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania.