MABORESHO MIUNDOMBINU YA MAJI CHANGANYIKENI KAZI INAENDELEA
22 Apr, 2024
Maboresho ya miundombinu ya usambazaji maji katika eneo la Pori la Jeshi Changanyikeni Wilaya ya Ubungo inaaendelea kutekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kwa lengo la kuboresha huduma ya Majisafi.
Kazi hii inahusisha ulazaji wa bomba za inchi 8 kwa umbali wa Kilomita 2 kwa lengo la kubadilisha sehemu ya bomba iliyoathirika ili kuondokana na upotevu wa maji.
Kukamilika kwa kazi kutaimarisha huduma kwa wakazi wa maeneo ya;
Mti Pesa, Goba, Hekima, Kibululu, Tegeta A, Rastanza Juu, Rastanza Chini, West River
Aidha, DAWASA inaendelea kuwakumbusha wateja wake kuendelea kuhifadhi maji kwa kipindi hichi cha matengenezo.