KISARAWE WABORESHEWA HUDUMA ZA MAJI - PWANI
19 Mar, 2024
Kazi ya maboresho huduma ya maji ikiendelea katika maeneo ya Kimani, na Kigogo kwa lengo la kuongeza msukumo wa maji katika maeneo yanayopata huduma kwa kiasi kidogo.
Maboresho yanahusisha kubadilisha mabomba yenye kipenyo cha inchi 3 na kuweka bomba za inchi 6 na 7 itakayoboresha upatikanaji wa huduma kwa wananchi takribani 500 katika mitaa ya Kimani, Msikiti wa Mabati, Pugu kona, Bane kwa Maswi, Kigogofresh B, Serikali ya mtaa Kigogofresh na Big brother.