KIJICHI NA TOANGOMA WANUFAIKA NA HUDUMA ZA DAWASA
24 Apr, 2024
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imetoa vifaa vya maunganisho mapya ya huduma ya majisafi kwa wateja wa maeneo ya Kijichi, Kibondemaji, Kilungule, Chamazi, Mbagala, Mianzini na Toangoma. waliokamilisha taratibu za kupata huduma.
Zoezi limeenda na utoaji wa elimu mbalimbali ikiwa ni pamoja na elimu ya utunzaji miundombinu ya maji, matumizi sahihi ya maji, njia rasmi za mawasiliano na Mamlaka, njia za malipo ya ankara na huduma nyingine zitolewazo na DAWASA.