Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
KIJICHI HADI KIBURUGWA WAITWA MAUNGANISHO HUDUMA YA MAJI - MBAGALA
13 Feb, 2024
KIJICHI HADI KIBURUGWA WAITWA MAUNGANISHO HUDUMA YA MAJI - MBAGALA

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) inawataarifu wakazi wa maeneo ya Kijichi, Mbagala Kuu, Kibonde Maji, Kichemchem, Bughudadi, Makuka, Kimbangulile, Nzasa, Juhudi, Kingugi na Kiburugwa kuwa inaendelea na zoezi la ugawaji na utoaji wa vifaa vya maunganisho mapya ya huduma ya majisafi kupitia ofisi ya kihuduma DAWASA Mbagala

Sambamba na zoezi hilo, elimu ya huduma za maji, njia za malipo pamoja na mawasiliano na Mamlaka zinatolewa kwa wateja wapya.
Takribani Wananchi 100 katika maeneo tajwa watanufaika na huduma ya majisafi baada ya maunganisho kukamilika.

Endelea kuwasiliana na DAWASA kupitia kituo cha huduma kwa wateja namba 0800110064 (Bure) au 0734302352 (DAWASA Mbagala).