Kazi ya matengenezo ya bomba la inchi 10’ kudhibiti upotevu wa maji, katika eneo la Mbezi kwa Kayombo kata ya Mbezi
15 Aug, 2023
Kazi ya matengenezo ya bomba la inchi 10’ kudhibiti upotevu wa maji, katika eneo la Mbezi kwa Kayombo kata ya Mbezi ikiendelea kutekelezwa na mafundi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA)
Kukamilika kwa kazi hii kutaboresha huduma ya majisafi kwa wakazi takiribani 200 wa Mbezi mazulu, Maendeleo, Njia Panda Makabe, Family Park, Amani, kwa Robert,Mji Mpya, Upendo Utawale,Twiga, Baraka,Summit , Muhimbili, Uzunguni, Mbezi Luis na Lugugwe.