MRADI WA USAFI WA MAZINGIRA PSSSF WASHIKA KASI
05 Sep, 2023
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) ndugu Kiula Kingu ametembelea na kukagua utekelezaji wa mradi wa Usafi wa Mazingira PSSSF Sinza-Kijitonyama wenye lengo la kumaliza uchafuzi wa Mazingira katika eneo hilo.
Mradi wa wa Usafi wa Mazingira PSSSF Sinza-Kijitonyama unategemea kukamilika mwezi Septemba 2023 na kuhudumia wateja takribani 1000.