Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
JE WEWE NI MKAZI WA UKONGA NA PUGU 
15 Sep, 2023
JE WEWE NI MKAZI WA UKONGA NA PUGU 

Habari njema kwa wakazi wa Kata ya Gongo la Mboto na Pugu, kuwa ofisi za DAWASA - UKONGA inaendelea na zoezi la utoaji wa vifaa vya maunganisho mapya ya huduma ya majisafi kwa wateja wake. 

Zaidi ya wateja 54 wa maeneo ya Gongo la Mboto, Ulongoni B, Mazizini, Viwege, Bangulo, Pugu, Pugu Stesheni, Kwa Rais, Pugu Mpakani na Pugu Mnadani wamepatiwa vifaa vya maunganisho mapya ya majisafi. 

Zoezi la utoaji wa vifaa vya maunganisho mapya lilienda sambamba na utoaji wa elimu ya utunzaji wa miundombinu ya vifaa vya majisafi, matumizi sahihi ya maji, njia za mawasiliano pamoja na huduma nyingine zitolewazo na DAWASA. 

Kwa msaada na taarifa zaidi wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja namba 0800110064 (Bure) au 0739-038493 (DAWASA - Ukonga).