Je wewe ni Mkazi wa Salasala, Mbweni, Kunduchi, Bunju na Tegeta na uliomba huduma ya Maji DAWASA!
15 Sep, 2023
Habari njema kwa wakazi wa maeneo tajwa kuwa Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) inaendelea na zoezi la kugawa vifaa vya maunganisho mapya ya huduma ya majisafi kwa wateja walioomba huduma.
Fika ofisi za DAWASA-Tegeta zilizopo eneo la … uweze kuhudumiwa na kupata elimu ya utunzaji miundombinu ya maji, matumizi sahihi ya maji, njia za malipo ya ankara na huduma nyingine za Mamlaka.
Kwa msaada na taarifa zaidi wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja namba 0800110064 (Bure) au 0738096084 (DAWASA Tegeta)