Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
JAMII YA WAFUGAJI NA WAKULIMA WAASWA KUJIEPUSHA UHARIBIFU WA MIUNDOMBINU YA MAJI
05 Sep, 2023
JAMII YA WAFUGAJI NA WAKULIMA WAASWA KUJIEPUSHA UHARIBIFU WA MIUNDOMBINU YA MAJI

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imetoa elimu kwa wananchi jamii ya wafugaji na wakulima katika Vijiji vya Chamakweza, Magindu na Mizuguni vilivyopo katika Halmashauri ya Chalinze na Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Vijijini.

Elimu inayotolewa imelenga kuwasihi wananchi kulinda miundombinu ya maji pamoja na kuwa mabalozi wa ulinzi na utunzaji wa miundombinu ya maji.

Akizungumza na wananchi wa Vijiji hivyo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Vijijini, Mhe. Erasto Mpangala ameipongeza Mamlaka kwa kutoa elimu ya utunzaji wa miundombinu ya maji kwa jamii za wafugaji na wakulima wa vijiji hivyo.

“Naipongeza Serikali kupitia Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kwa kazi ya utoaji wa elimu juu ya ulinzi wa miundombinu ya maji pamoja na uboreshaji wa hali ya upatikanaji wa huduma ya maji katika Vijiji vyetu, nina imani maeneo mengi zaidi yatanufaika na utekelezaji wa miradi inayoendelea kutekelezwa na DAWASA” Ameeleza Mhe. Erasto

Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka DAWASA, Ndugu Elizabeth Eusebius ameeleza kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imewekeza fedha nyingi katika sekta ya maji ili kutekeleza miradi, hivyo ni wajibu wa kila mnufaika kulinda na kuitunza miundombinu ya maji.

"Nitoe rai kwa wananchi kuisaidia Mamlaka katika kulinda na kutunza miundombinu ya maji ili kupata huduma iliyo bora na endelevu" amesema ndugu Elizabeth.

Ndugu Elizabeth Eusebius ameeleza kuwa DAWASA imejipanga kupunguza upotevu wa maji kutoka asilimia 30 mpaka kufikia asilimia 25 kwa mwaka wa fedha 2023/2024 hivyo Mamlaka peke yake haiwezi kufikia lengo hilo bila kushirikiana na wananchi.

Nae Mhandisi wa Uendeshaji na matengenezo mkoa wa kihuduma DAWASA Chalinze, Mhandisi Nkilo Mushi ameeleza kuwa huduma ya maji kwa Vijiji vya Chamakweza,Magindu,Mizuguni  na maeneo ya jirani imeimarika ikilinganishwa na hapo awali.

"Utekelezaji wa mradi wa maji Chalinze awamu ya tatu pamoja na mradi wa maji Mlandizi -Chalinze-Mboga umeimarisha upatikanaji wa huduma ya maji katika maeneo hayo na kazi ya kusambaza maji haya katika maeneo mengi zaidi inaendelea" ameeleza

Mhandisi Mushi ameeleza kuwa mpango uliopo sasa ni kusogeza huduma ya majisafi kwa wananchi na vituo vya huduma za kijamii zilizopo mbali na miundombinu ya DAWASA pamoja na kuboresha vioski vya maji ili kuhakikisha huduma inazidi kuimarika. Hivyo ametoa rai kwa wananchi wanaohitaji huduma ya maji kuwasilisha maombi rasmi katika ofisi za DAWASA ili kuunganishiwa huduma.

Ndugu Amos Enock, Afisa Sheria wa DAWASA nae amewasisitiza wananchi wanaoishi Chamakweza na Magindu kutumia huduma ya maji kwa kuzingatia sheria ya huduma ya Maji na Usafi wa Mazingira Na. 5 ya mwaka 2019.

"Niwasisitize ndugu wananchi iwapo kuna uvujaji wa maji, wizi wa maji au uharibifu wa miundombinu ya maji ya Mamlaka basi ni vyema kufika ofisi za DAWASA Chalinze au kutoa taarifa kupitia namba za huduma kwa wateja” ameeleza Ndugu Amos

Filemon Tegirii mkazi wa Chamakweza ameishukuru DAWASA na kuipongeza kwa jitihada za kutoa elimu na kuishirikisha jamii haswa kuhusu sheria za uharibifu wa miundombinu ya maji kwani elimu hii itasaidia wananchi kuwa mabalozi