Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
HUDUMA KWA WAKAZI WA TUMBI-KIBAHA ZAIMARISHWA
22 Apr, 2024
HUDUMA KWA WAKAZI WA TUMBI-KIBAHA ZAIMARISHWA

Kazi ya uchimbaji na ulazaji wa bomba la inchi 12 kwa umbali wa kilomita moja ikitekelezwa na mafundi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira DAWASA Kupitia mkoa wa kihuduma DAWASA Kibaha kwa lengo la kuongeza upatikanaji wa huduma katika Kata ya Tumbi-Kibaha, Mkoani Pwani. 

Kukamilika kwa kazi hii kutaboresha upatikanaji wa huduma ya maji kwa kuongeza msukumo wa maji kwa wakazi 1,650 wa maeneo ya Boko temboni, Boko mnemela, Boko timiza, Mwanalugali, Sofu, Masaki, Mkarambati, Kibaoni na Mpiji.