Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
HABARI NJEMA KWA WAKAZI WA MAKONGO HADI KILUNGULE 
06 Sep, 2023
HABARI NJEMA KWA WAKAZI WA MAKONGO HADI KILUNGULE 

Habari njema kwa wakazi wote wa maeneo ya Makongo, Goba, Tegeta A, Mbezi Louis, Matosa, Makabe, Kimara Baruti na Kilingule kuwa ofisi za DAWASA MAKONGO inaendelea na zoezi la utoaji wa vifaa vya maunganisho mapya ya huduma ya majisafi.

Zoezi hilo linaenda sambamba na utoaji wa elimu ya utunzaji miundombinu ya maji, matumizi sahihi ya maji, njia rasmi za mawasiliano na malipo ya ankara na huduma nyingine zitolewazo na DAWASA. 

Takribani wateja zaidi ya 50 wa maeneo hayo wanatarajia kuanza kunufaika na huduma ya majisafi.

Kwa msaada na taarifa zaidi wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja namba 0800110064 (Bure) au 0736602601 (DAWASA Makongo)