Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
HABARI NJEMA KWA WAKAZI WA MAILI MOJA HADI VISIGA
15 Sep, 2023
HABARI NJEMA KWA WAKAZI WA MAILI MOJA HADI VISIGA

Habari njema kwa wakazi wote wa maeneo ya Picha ya ndege, Ungindoni, Tangini, Muheza, Mailimoja shule, Miembesaba A na B, Kongowe bamba, Kongowe forest, Visiga, Garagaza, Kimbani, Kwa mfipa, Mwendapole A na B, Kata, Zegereni, Maili 35, Visiga madafu, Visiga kipofu na  Karabaka kuwa ofisi za DAWASA KIBAHA inaendelea na zoezi la utoaji wa vifaa vya maunganisho mapya ya huduma ya majisafi.

Pamoja na zoezi hilo, elimu mbalimbali zinatolewa ikiwa ni pamoja na elimu ya utunzaji miundombinu ya maji, matumizi sahihi ya maji, njia rasmi za mawasiliano na malipo ya ankara na huduma nyingine zitolewazo na DAWASA. 

Jumla ya wateja 117 wa maeneo hayo wanatarajia kuanza kunufaika na huduma ya majisafi.

Kwa msaada na taarifa zaidi wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja namba 0800110064 (Bure) au 0734 460 022 (DAWASA Kibaha).