HABARI NJEMA KWA WAKAZI WA MAILI MOJA HADI MISUGUSUGU
06 Sep, 2023
Habari njema kwa wakazi wote wa maeneo ya Maili moja, Tumbi, Mkoani, Miembesaba, Kongowe, Visiga na Misugusugu kuwa ofisi za DAWASA KIBAHA inaendelea na zoezi la utoaji wa vifaa vya maunganisho mapya ya huduma ya majisafi.
Utoaji wa vifaa vya maunganisho mapya huendana sambamba na utoaji wa elimu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na elimu ya utunzaji miundombinu ya maji, matumizi sahihi ya maji, njia rasmi za mawasiliano, njia za malipo ya ankara na huduma nyingine zitolewazo na DAWASA.
Jumla ya wateja 143 wa maeneo tajwa wanatarajiwa kuanza kunufaika na huduma ya majisafi.
Kwa msaada na taarifa zaidi kuhusu huduma wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja namba 0800110064 (Bure) na 0734 460 022 (DAWASA Kibaha).