GOBA MPAKANI WABORESHEWA HUDUMA YA MAJI
15 Sep, 2023
Zoezi la kulaza na bomba ya inchi 6, 4 na 3 ikitekelezwa kwa lengo la kusogeza huduma ya Majisafi kwa wakazi wa Goba mpakani ambao ni wanufaika wa mradi wa usambazaji maji Makongo hadi Bagamoyo
Kazi hii inayotekelezwa na mafundi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA)- Makongo inalenga kufikisha huduma kwa wakazi takribani 500 wa eneo hilo.
Mradi wa maji Makongo hadi Bagamoyo ni miongoni mwa mradi wa kimkakati uliotekelezwa na Mamlaka kwa lengo la kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji hasa kwa wakazi wa Goba.