Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
ELIMU YA MATUMIZI YA DIRA ZA MALIPO YA KABLA YATOLEWA POLISI OYSTERBAY
22 Apr, 2024
ELIMU YA MATUMIZI YA DIRA ZA MALIPO YA KABLA YATOLEWA POLISI OYSTERBAY

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imeendesha zoezi la kutoa elimu katika makazi ya watumishi wa Jeshi la Polisi Oysterbay Wilaya ya Kinondoni ikiwa ni muendelezo wa matumizi ya mita za kabla zilizofungwa kwa wateja wa Mkoa wa Dar es Salaam.

DAWASA imefunga mita za malipo ya kabla takribani 50 za huduma ya malipo ya kabla (Pre-paid meters) katika makazi ya watumishi hao.

Lengo la kufunga mita hizo ni kuangalia na kupima ufanisi wake kuelekea mabadiliko ya kuanza kutumia rasmi mita za huduma ya malipo ya kabla unaotarajia kuanza hivi karibuni.