Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
DAWATI LA HUDUMA KWA WATEJA LAWAFIKIA WAKAZI WENGI KINONDONI
18 Apr, 2024
DAWATI LA HUDUMA KWA WATEJA LAWAFIKIA WAKAZI WENGI KINONDONI

Katika kuendelea kuadhimisha Wiki ya Maji Duniani inayofanyika tarehe 16 - 22 kila mwaka, Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kupitia dawati lake la huduma kwa wateja imewafikia na kuwasikiliza wateja wengi sambamba na kupatiwa elimu juu ya huduma za DAWASA.

Dawati  la huduma kwa Wateja limefunguliwa katika Kituo cha Kusukuma Maji katika Kata ya Wazo, Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Maadhimisho ya Wiki ya Maji Duniani  mwaka  2024 imebeba kauli mbiu isemayo "Uhakika wa Maji kwa Amani na Utulivu"