DAWASA YAWASHIRIKISHA WAKAZI VIJIBWENI MRADI WA USAFI WA MAZINGIRA
03 Jul, 2023
DAWASA YAWASHIRIKISHA WAKAZI VIJIBWENI MRADI WA USAFI WA MAZINGIRA
Watumishi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) wakijenga uelewa kwa wakazi wa Mkwajuni, kata ya Vijibweni, Wilaya ya Kigamboni ambao wananufaika na ujenzi wa mtambo wa kisasa wa kuchakata takatope unaojengwa katika eneo la Vijibweni.
Ujenzi wa mtambo wa kuchakata takatope Vijibweni uko katika hatua za awali ambapo ukikamilika utakuwa na uwezo wa kuchakata lita 50,000 kwa siku. Mitambo 8 ya kisasa ya kuchakata takatope inayojengwa kupitia mradi wa Uboreshaji Usafi wa Mazingira imewekwa kimkakati katika Wilaya ya Ilala, Temeke, Kinondoni, Ubungo na Kigamboni ili kupunguza umbali kati ya mteja na sehemu ya kutibu takatope.