DAWASA YAWAKUMBUSHA WATEJA UMUHIMU WA USOMAJI MITA SHIRIKISHI - TEMEKE
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kupitia Mkoa wa Kihuduma DAWASA- Temeke imeendelea kuwakumbusha wateja wake juu ya umuhimu wa usomaji mita shirikishi wakati zoezi la usomaji mita unaoendelea.
Afisa ankara DAWASA Temeke, Ndugu Rashid Mohamed amesema usomaji mita shirikishi husaidia mteja kufahamu matumizi yake ndani ya mwezi husika na hivyo kusaidia katika uandaaji wa bili na kupunguza changamoto za kihuduma.
"Ushirikiano kati ya wateja na DAWASA ni muhimu ili kurahisisha zoezi la usomaji mita, kwa kufanya hivyo pia tunapunguza changamoto mbalimbali." amesema.
Ndugu Mohamed amesema DAWASA inaendelea na elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa kushiriki katika zoezi la usomaji mita.
Mkoa wa kihuduma Temeke una jumla ya wateja takriban 15,000 na unahudumia Kata za Yombo vituka, Buza, Temeke, Makangarawe, Keko/Chang'ombe, Kiwalani, Tandika, Sandali, Kurasini na Mtoni