Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
DAWASA YAWAKUMBUKA WAHITAJI MWANANYAMALA
05 Sep, 2023
DAWASA YAWAKUMBUKA WAHITAJI MWANANYAMALA

Katika hatua ya kuthamini mchango wa wahitaji katika jamii, Mamlaka ya Majisafi na Usafi na Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imetoa misaada mbalimbali katika wodi ya wazazi na watoto njiti katika hospitali ya rufaa ya Mwananyamala kwa lengo la kukidhi mahitaji ya makundi hayo.

Akizungumza wakati wa utoaji wa misaada hiyo, Meneja huduma kwa wateja DAWASA, Bi. Doreen Kiwango ameeleza kuwa ni utaratibu wa Mamlaka kurudisha fadhila kwa jamii kupitia njia mbalimbali ili kuonesha mchango wa Mamlaka kwenye jamii inayoihudumia.

"Huu ni utaratibu wa Mamlaka wa kurudisha kwa jamii kwa kuyakumbuka makundi maalumu kwa njia mbalimbali," ameeleza Kiwango.

Naye Msimamizi Mkuu wa wa Kitengo cha Mama na mtoto hospitali ya Mwananyamala, Bi Dolphina Simon ameishukuru sana DAWASA kwa msaada huo kwani hospitali imekuwa na uhitaji mkubwa wa vitu misaada ya kibinadamu..

"Niwashukuru sana DAWASA kwa msaada waliotoa, nitoe wito kwa Taasisi nyingine na watu binafsi kuendelea kukumbuka wahitaji katika maeneo tofauti, hata vitabu vya dini vinatukumbusha katika hili" amesema Dolphina.

Naye, Bi. Luiza Alex ambae ni mzazi katika wodi hiyo ameishukuru DAWASA kwa fadhila hizo na kuomba uwe ni muendelezo kwani bado kuna uhitaji mkubwa na wenye changamoto wanaohitaji msaada ni wengi katika jamii.

Imekuwa ni desturi ya Mamlaka kurudisha fadhila kwa jamii yenye uhitaji ili kuimarisha uhusiano kati ya Taasisi na jamii.