DAWASA YAWAKUMBUKA WAHITAJI KIPUNGUNI - ILALA
16 Feb, 2024
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) imekabidhi mahitaji ya kibinadamu kwa kituo cha watoto wanaoishi katika mazingira magumu kilichopo mtaa wa Kipunguni mashariki, kata ya Kipunguni katika wilaya ya Ilala.
Msaada hiyo ni sehemu ya jitihada za Mamlaka katika kutambua na kujali uwepo na umuhimu wa makundi haya maalum kwenye jamii.
DAWASA imekuwa ikichangia jamii zenye uhitaji kwa kutambua umuhimu wa huduma yake katika maisha ya Binadamu.