Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
DAWASA YAWAKUMBUKA MAKUNDI MAALUM MUHIMBILI ILALA
19 Jan, 2024
DAWASA YAWAKUMBUKA MAKUNDI MAALUM MUHIMBILI ILALA

DAWASA YAWASHIKA MKONO WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM MUHIMBILI

Mamlaka ya Majisafi na Usafi na Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imekabithi mahitaji maalum katika wodi ya wazazi na watoto njiti katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili kama sehemu ya kutambua wenye uhitaji na kurudisha kwa jamii inayoihudumia.

Akizungumza wakati wa utoaji wa misaada hiyo, Afisa Mawasiliano msaidizi DAWASA, Ndugu Neema Manyama ameeleza kuwa misaada hii inalenga kuwasaidia wazazi kukidhi mahitaji ya watoto wao kipindi wawapo hospitali kwa kutambua muda mrefu watakaoutumia katika matibabu ya watoto.

"Umekuwa ni utaratibu kwa Mamlaka kutoka misaada kwa kuyakumbuka makundi mbalimbali ndani ya jamii kwa lengo la kusaidia kutatua changamoto zilizopo za kibinadamu," ameeleza Neema. 

Akipokea msaada huk, Afisa Muuguzi kutoka wodi ya wazazi Muhimbili, Miriam Shauri ameishukuru DAWASA kwa mchango huo na kusisitiza jamii na makundi mengine yahitokeze zaidi kwani bado hospitali ina uhitaji zaidi wa misaada mbalimbali. 

"Niwashukuru sana DAWASA kwa msaada waliotoa, changamoto ni nyingi, ila kwa hili mlilolifanya leo litatusaidia katika kuwahudumia watoto tulionao" aliongezea

 Pendo Charles ambae ni miongoni mwa mzazi katika wodi hiyo ameishukuru DAWASA kwa mchango na kuomba uwe ni muendelezo kwani uhitaji bado ni mkubwa na kutoa wito kwa Taasisi nyingine na watu binafsi kukumbuka wahitaji katika maeneo tofauti," amesema Ndugu Pendo.